1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Wafuasi wa mpinzani wa Modi waingia mitaani kutaka aachiwe

23 Machi 2024

Mamia ya waandamanaji waliingia mitaani leo kwenye mji mkuu wa India, New Delhi, kushinikiza kuachiwa huru kwa moja ya wapinzani wakuu wa Waziri Mkuu Narendra Modi aliyekamatwa mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/4e3e9
Waziri Kiongozi wa jimbo la Delhi Arvind Kejriwal
Waziri Kiongozi wa jimbo la Delhi Arvind Kejriwal na mpinzani wa waziri mkuu wa India Narendra Modi.Picha: BIJU BORO/AFP/Getty Images

Arvind Kejriwal, ambaye ni waziri kiongozi wa jimbo la Delhi na moja ya wanasiasa mashuhuri nchini India, alikamatwa siku ya Alhamisi na Idara ya kusimamia sheria ya serikali ya shirikisho.

Chombo hicho kinachodhibitiwa na serikali ya Modi, kinakituhumu chama cha Kejriwal na mawaziri wake kwa kupokea hongo ya kiasi dola milioni 12 kutoka wazalishaji vileo kiasi miaka miwili iliyopita.

Chama cha mwanasiasa cha Aam Aadmi kinayapinga madai hayo na kimesema Kejriwal  atabakia kuwa waziri kiongozi wa Delhi wakati kinapeleka malalamiko yake mahakamani.

Wafuasi wa kiongozi huyo wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumdhihaki Modi, waliingia mitaani kulaani kile wamekitaja kuwa "udikteta" na kushinikiza Kejriwal aachiwe huru.