1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafaransa wamchagua rais kesho

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8P

PARIS:

Watetezi mashuhuri kabisa katika uchaguzi wa hapo kesho wa rais nchini Ufaransa, walifanya jana kampeni yao ya mwisho kuvutia kura upande wao.Usoni kabisa ni mtetezi wa chama-tawala cha kiConservative Nocolas Sarkozy na Bibi Segolene Royal wa chama cha kisoshalist.Nafasi ya tatu anafuatia Francois Bayrou wa jukwaa la kati na Jean-Marie le Pen,mkongwe wa mrengo wa kulia kabisa.Ikiwa kama inavyotarajiwa hakuna atakeibuka na ushindi duru ya kwanza hapo kesho, duru ya pili imepangwa Mei 6.