Wafaransa 6 walioshtakiwa Chad warudi nyumbani
29 Desemba 2007Matangazo
PARIS
Wafanyikazi sita wa kifaransa wa shirika la kutoa misaada la Zoe Ark walioshtakiwa kwa kujaribu kuwaiba watoto 103 kutoka nchini Chad wameshawasili nchini Ufaransa.Mapema wiki hii
Mahakama ya Chad iliwahukumu kifungo cha miaka minane jela na kazi ngumu wafanyikazi hao wanne wakiume na wawili wa kike.Serikali ya Ufaransa iliomba Chad kuwarudisha raia hao wa Ufaransa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1976 ambayo inaruhusu raia wa Ufaransa kutumikia kifungo nchini mwao.Wafanyikazi hao sita walidai kwamba nia yao ilikuwa kuwasaidia na kuwaokoa watoto yatima lakini kilichobainika ni kuwa wengi wa watoto waliokuwa wamewachukua bado familia zao ziko hai.