MigogoroYemen
Waasi wa Houthi wakiri kushambulia meli ya Uholanzi
1 Oktoba 2025
Matangazo
Meli hiyo ya mizigo MV Minervagracht ilishambuliwa na kombora siku ya Jumatatu lililowajeruhi watu wawili na kusababisha moto, hii ikiwa ni kulingana na mmiliki wa meli.
Waasi hao wamesema kwenye taarifa iliyotangazwa na shirika lake la habari la Saba kwamba waliilenga meli hiyo kwa sababu kampuni inayomiliki ilikiuka uamuzi wa kupiga marufuku kuingia katika bandari za Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Waasi hao wanaoungwa mkono na Iran wanafanya mashambulizi ya meli za kibiashara kama ishara ya kuwaunga mkono Wapalestina katikati ya vita vya Israel na Hamas huko Gaza.