Waandishi wa DW wasimulia hadithi za maisha yao: #ninakotokea | Media Center | DW | 02.10.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Media Center

Waandishi wa DW wasimulia hadithi za maisha yao: #ninakotokea

Katika mfululizo wa vidio fupi, tunataka kuwatambulisha kwako baadhi ya waandishi wetu usikie kuhusu maisha yao na namna walivyochagua kukifanya wanachokifanya.

Tazama vidio 01:02

Elizabeth Shoo

Ndoto zinavyosaidia kuunda maisha ya kikazi

DW ndiyo shirika la utangazaji la kimataifa la Ujerumani likiwa na maelfu ya waandishi kutoka kote ulimwenguni. Simulizi zao binafsi zinamulika safari ambayo wengi wao wameifanya ili kufanya kazi katika chombo cha habari cha kimataifa. Ufuatiliaji wa historia yao unasaidia kuwapa mtazamo tofauti wa sio tu namna mandhari yanavyobadilika, lakini pia kuiendeleza. Kupitia #ninakotokea, tunataka kukuonesha namna vivuli hivi vilivyowajenga waandishi habari wetu na kuwafanya kuwa vile walivyo sasa.

Je, wenyeji wa Bavaria wanazungumza Kiswahili?

Elizabeth Shoo alizaliwa nchini Ujerumani lakini alilelewa Tanzania, hivyo ana mizizi katika mabara yote mawili – Ulaya na Afrika. Ingawa anasema maeneo hayo yote kwake ni nyumbani, moyoni mwake anajihisi zaidi kama Mtanzania. Baada ya kurejea Ujerumani kwa ajili ya masomo ya juu, alishiriki katika programu ya mafunzo ya Chuo cha DW – DW Akademie – na hakuondoka tangu wakati huo. Anasema hisia zake za nyumbani zinaweza kubadilika mara moja na wakati wowote. Mara anapowasili Tanzania, au vinginevyo, kuna mabadiliko yanayotokea moja kwa moja: Kutoka nchi yake ya kuzaliwa inayoheshimu muda na yenye  utaratibu mzuri, hadi nchi ya mababu na mabibi zake angavu yenye mvuto na shughuli nyingi. Ni uelewa huu wenye kujitokeza wa tamaduni mbili unaompa mtazamo wa kipekee wa dunia. Kwa sasa anafanya kazi na timu ya mitandao ya kijamii ya Idara ya Habari ya DW na pia redioni katika Idhaa ya Kiswahili.

Mbali na nyumbani

Mwanzoni mwa 2017, Edith Kimani aliondoka kuja Ujerumani kuanza maisha mapya na kazi mjini Berlin, kama mtangazaji wa habari wa DW. Aliacha mashabiki wengi nchini Kenya lakini alileta uzoefu wa miaka saba kama ripota na mtangazaji wa habari wa moja ya vituo vikubwa kabisa vya televisheni nchini Kenya, KTN. 

Tazama vidio 01:07

Edith Kimani

Mwaka 2009, Edith alianza kazi baada ya kushinda mashindano ya KTN kutafuta mtangazaji habari kijana mwenye kipaji zaidi nchini Kenya. Kimani, mwenye mapenzi makubwa na mazingira, aliongoza mdahalo wa DW katika Jukwaa la Kimataifa la Kiuchumi kuhusu Afrika, juu ya mada ya nishati jadidifu. Kabla ya kuja Ujerumani, alikuwa ripota wa DW katika kanda ya Afrika Mashariki na mwendeshaji wa kipindi cha Eco@Africa cha DW.

‘Bibi' mchapakazi na mpambanaji

Debarati Guha amepewa jina "bibi” na timu ya uhariri ya Idhaa ya Kibengali kwa sababu anajali kuhusu wengine na anajaribu kuelewa wasiwasi na matatizo yao. Anatumia kila fursa alio nayo kuhadithia simulizi za maisha ya wanawake na changamoto zao. Ni muhimu kwake kwamba watu duniani kote wanajifunza kuhusu hofu na wasiwasi wa watu nchini Bangladesh na India. Alizaliwa Kolkata, ingawa wazazi wake wanatokea Bangladesh.

Tazama vidio 01:13

Debarati Guha

Hivyo mara nyingi alijichukulia kama Mbengali kuliko kitu chochote kingine na kama binti ya mwanasheria, alijenga moyo wa mapambano na mapenzi katika siasa akiwa na umri mdogo. Ameishi Ujerumani tangu 2005. Alihitimu shahada yake ya uzamili na shahada ya uazmili katika Falsafa ya Sayansi ya Siasa kutoka chuo kikuu cha Nehru, na alifanya kazi kama msaidizi wa mwandishi wa Asia wa gazeti la Frankfurter Allgemeine mjini New Delhi. Baadae alihitimu programu ya mafunzo ya DW katika uandishi wa mtandaoni, redio na televisheni, na amekuwa akiongoza idhaa ya Kibengali tangu 2013.

Kutoka kusini Marekani hadi moyo wa Ulaya?

Kama muongozaji wa kipindi cha "The Day with Brent Goff” na Mtangazaji mkuu wa Habari wa idhaa ya Kingereza ya DW, Brent Goff anajua kwamba, katika zama za masimulizi ya mashaka na habari za uongo, uandishi unaozingatia viwango ni muhimu zaidi kuliko ilivyowahi kutokea.

Tazama vidio 01:09

Brent Goff

Alikulia katika vijiji vya North Carolina, na kazi yake ya kwanza katika uandishi wa televisheni ilikuwa katika kituo kidogo cha televisheni mjini Missouri. Lakini lengo lake lilikuwa kubwa na baada ya kuhitimu shahada yake ya uzamili katika chuo kikuu cha Georgetown kupitia ufadhili wa programu ya Fulbright na kufanya kazi kama mtengenezaji wa vipindi wa CNN mjini Berlin, alifahamu kuwa habari za kimataifa ndiyo mahala pake. Alijiunga na DW mwaka 2000 na tangu wakati huo amekuwa mmoja wa watangazazaji maarufu zaidi. Katika chumba cha habari mjini Berlin na kwa watazamaji wake duniani kote, Brent anajulikana kwa uchapakazi wake na uthabiti katika uandishi.

Sauti ya mapinduzi yazungumza kutoka mbali

Yosri Fouda ni mmoja wa waandishi maarufu zaidi wa habari za uchunguzi nchini Misri. Wakati wa vuguvugu la Mapinduzi ya Uarabuni, alidhani taifa hilo lilikuwa linaelekea kwenye mapinduzi ya utangamano. Lakini mara baada ya hapo wimbi likageuka na ukandamizaji ulioongezeka dhidi ya vyombo vya habari ukamlazimu kuondoka nchini humo.

Tazama vidio 01:11

Yosri Fouda

Ili kuendelea kuzungumzia kwa uhuru zaidi masuala muhimu ya kanda yake na watu wake, Yosri alikuja Ujerumani kuwa muongozaji DW. Katika kipindi chake cha kila wiki cha "Fifth Estate” - Mhimili wa tano, Yosri anachanganya uchambuzi yakinifu wa habari na ripoti za uchunguzi vinavyoipa hadhira ya ulimwengu wa Kiarabu, mtazamo huru kuhusu musuala muhimu. Yosri alianza kazi kama ripota wa BBC na alikuwa mkuu wa ofisi ya Aljazeera mjini London. Katika kituo cha utangazaji cha Misri cha ONTV wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya Uarabuni, alikuwa anajulikana kama "sauti ya mapinduzi.”

 

Sauti na Vidio Kuhusu Mada