1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Vyama vya Afrika Kusini vyajadii kuunda serikali ya mseto

10 Juni 2024

Vyama vya Afrika Kusini Jumatatu hii vinajadili mpango wa kuunda serikali ya mseto huku Rais Cyril Ramaphosa akitoa wito kwa vyama vyote kufanya kazi kwa pamoja.

https://p.dw.com/p/4gsLm
Afrika Kusini | Cyril Ramaphosa
Vyama nchini Afrika Kusini vyajadiliana juu ya kuunda serikali ya msetoPicha: Jerome Delay/AP/picture alliance

Chama cha Ramaphosa cha African National Congress (ANC) kilipata asilimia 40 ya kura , kiwango cha chini zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kwa demokrasia mwaka 1994, na sasa kinahitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili kutawala.

Ramaphosa amesema wakati Afrika Kusini ikijiandaa kwa utawala mpya wa kidemokrasia, pande zote zinahitaji kufanya kazi pamoja ili kuendeleza kasi ya mageuzi, ukuaji wa uchumi na mabadiliko.

Chama cha ANC tayari kimedokeza kinataka kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kundi pana la vyama vya upinzani, kuanzia mrengo wa kulia hadi mrengo mkali wa kushoto.