1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Umoja wa Afrika wakutana Nouakchott

Oumilkheir Hamidou
2 Julai 2018

Mkutano wa 31 wa viongozi wa Umoja wa Afrika unaendelea mjini Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania. Mada kuu mkutanoni ni jinsi ya kupiga vita rushwa. Hata hivyo migogoro inayolikaba bara hilo nayo pia itajadiliwa.

https://p.dw.com/p/30fDH
Mauritanien AU Gipfel
Picha: Getty Images/A.O.M.O.Elhadj

 

"Imesalia miezi 18 tu hadio mwaka 2020,muda uliowekwa na viongozi wa taifa na serikali wa kuweka chini silaha na kulitakasa bara la Afrika na balaa la migogoro"amesema mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alipokuwa akifungua mkutano huo mkuu wa 31 wa Umoja wa Afrika mjini Nouakchott. Matamshi hayo yanawapa  nguvu wale wanaohoji kwamba hotuba za viongozi wa Afrika baadhi ya wakati haziambatani na ukweli wa mambo. Ukweli huo umebainika wakati wa maandalizi ya mkutano wa kilele pale makao makuu ya kikosi cha kulinda amani katika nchi za Sahel G-5 yalipohujumiwa mjini Savare nchini Mali.

Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki MahamatPicha: picture-alliance/AA/M. W. Hailu

Mbali na juhudi za kupiga vita rushwa masuala ya usalama yanakamata nafasi muhimu pia katika mkutano huo wa 31 wa viongozi wa Umoja wa Afrika.

Licha ya maazimio kaadhaa na taarifa zinazotolewa kila wakati viongozi wa Afrika wanapokutana, mizozo bado inaendelea, naiwe Sahara Magharibi, jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Somalia , katika jamhuri ya Afrika Kati au Sudan Kusini na kwengineko..

Mkurugenzi wa  kituo cha taaluma za mikakati huko Oumtounsy, El Boukhary Mohammed amesema katika mahojiano na DW vikosi vya kigeni pekee haviwezi kutatua peke yao mizozo ya ndani barani Afrika. Kanali huyo wa zamani wa jeshi la Mauritania anaendelea kusema:"Mataifa yanabidi yawajibike wenyewe.Yanabidi yasake yenyewe ufumbuzi wa matataizo yao.Taifa ambalo haliwezi kufumbua matatizo yake, ni taifa lililoshindwa."

Makubaliano ya amani ya Sudan Kusini yatiwa saioni mjini Khartoum
Makubaliano ya amani ya Sudan Kusini yatiwa saioni mjini KhartoumPicha: AFP/Getty Images

 Ishara za maumaini mema zaanza kuchomoza

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika utamalizika baadae leo.Viongozi wa Afrika wanatabasamu kidogo; baada ya matumaini ya kufikiwa makubaliano ya amani kati ya Ethiopia na Eritrea, makubaliano ya amani yametiwa saini pia hivi karibuni mjini Khartoum kati ya mafahali wawili wa Sudan Kusini.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

MhaririJosephat Charo