1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi Serbia na Kosovo wakutana na wasuluhishi wa Ulaya

Sudi Mnette
2 Juni 2023

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti wamefanya mazungumzo ya ana kwa ana kwa lengo la kupunguza mvutano baina ya pande hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4S5f3
Moldawien | Gipfeltreffen der Europäischen Politischen Gemeinschaft | Marcron, Scholz Vucic und Osmani-Sadriu
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti wamekutana katika mkutano uliowahusisha Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ikiwa kandoni kabisa mwa  Mkutano wa Kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya wa huko Moldova.

Umoja wa Ulaya umekuwa katika jitihada ya kurejesha hali ya kidiplomasia baina ya pande hizo mbili hasimu ikiwa ni takribani miaka 15 baada ya Kosovo kujitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia. Katika miezi ya hivi karibuni kumeshuhudia kuongezeka kwa vurugu katika eneo lenye wakazi wenge wenye asilia ya Serbia kwa upande wa kaskazini mwa Kosovo.

Scholz: Warsbia na Wakosovo wajitenge na vurugu.

Moldawien Treffen Vjosa Osmani , Emmanuel Macron, Olaf Scholz
Rais Vjosa Osmani , Rais Emmanuel Macron, na Kansela Olaf Scholz Picha: Office of the President of Kosovo

Baada ya mkutano huo Kansela Scholz wa Ujerumani alisema ni muhimu kwa kila mmoja kufanya kila liwezekanalo kujiweka kando na machafuko. Kansela huyo pamoja na kutoeleza lolote kuhusu mafanikio ya mkutano huo lakini makubaliano yamejadiliwa na sasa yatapaswa kutekelezwa kwa lengo la kufikia suluhisho la mzozo.

Kasema huyo amesema katika hatua ya mwanzo kabisa yeye na Rais wa Ufaransa na wadau wengine kama vile  Josep Borrell wanajaribu sana kuhakikisha kwamba wanapunguza mvutano ambao sasa unazidi kuongezeka baina ya  Serbia na Kosovo.

Amenukuliwa na vyombo vya habari akisema "Tumezungumza juu ya hili kwa kina na umakini mkubwa na pia tumeelezea mtazamo wetu wa mambo kwa wale wanaohusika hapa. Na tutaona nini kitakachotokana na hatua hii. Lakini bila shaka ni jambo zito sana, na pia tumelichukulia kwa uzito mkubwa sana na kulazimika kufanya majadiliano haya hapa." alisema Kansela Scholz.

Vurugu zinaripotiwa katika maeneo ya kaskazini mwa Kosovo.

Wakati huohuo, Warsebia katika eneo tete la kaskazini mwa Kosovo wameendelea kufanya maandamano dhidi ya mameya wapya walioteuliwa katika eneo hilo. Mikusanyiko mkubwa ya watu ilifanyika mbele ya majengo ya manispaa katika miji ya  Zvecan, Leposavic na Zubin Potok.

Kwa mujibu wa taarifa ya jarida moja la mtandaoni Koha.Net, maandamano ya Alhamis yalikuwa ya amani. Lakini yale ya Jumatatu yalizusha vurugu katika mji wa Zvecan kati ya Warsbia na walinzi wa amani wa NATO, ambao wanaongoza jitihada ya usalama katika eneo hilo, hatua ambayo ilisababisha watu wanane wajeruhiwe wakiwemo walinzi hao 30.

Soma zaidi:Mzozo kati ya Kosovo na Serbia wazusha wasiwasi kwa Jumuiya ya Kimataifa

Maandamano yanayatokea katika kipindi hiki yanachochewa na hatua ya serikali kuwaweka mamea wapya katika maeneo ambayo yana idadi kubwa ya Waserbia. Kosovo ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia 2008, hatua ambayo hadi sasa Serbia imekataa kutambua.

Chanzo: DPA

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso Ibrahim Traore akizungumza na waandishi wa habari mjini Ouagadougou, Burkina Faso Oktoba 2, 2022
Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW
Nenda ukurasa wa mwanzo