1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vigogo waondolewa katika hatua ya mtoano

Bruce Amani
2 Julai 2018

Ni Kombe la Dunia ambalo linaendelea kushangaza na hasa kutokana na matokeo ya mechi. Miamba wa kandanda wameondoka katika njia ambayo sio wengi walitarajia

https://p.dw.com/p/30gS3
Fußball WM 2018 Spanien vs Russland
Picha: Reuters/A. Gea

Wenyeji Urusi walifanya kazi kweli kweli na kuwaondoa Uhispania kupitia mikwaju ya Penalti sawa na walivyofanya Croatia dhidi ya Denmark.

Mpaka sasa mechi mbili za robo fainali zimeshathibitishwa. Ijumaa tarehe 6 Uruguay watashuka dimbani dhidi ya Ufaransa, na kisha Jumamosi, tarehe 7, wenyeji Urusi watapambana na Croatia. Katika mechi nyingine mbili za robo fainali: Mshindi kati ya Brazil na Mexico atachuana na mshindi kati ya Ubelgiji na Japan. Kisha mshindi kati ya Sweden na Switzerland atamualika mshindi kati ya Colombia na England. 

Baadaye leo usiku, Ubelgiji wataangushana na Japan ambayo ina ndoto ya kutinga robo fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa. Narudi kwake Mtemi Ramadhan kupata tathmini yake, Mtemi, ni mechi ambayo ukiangalia kwenye karatasi, utajua tu ushindi ni wa Ubelgiji, lakini mechi za mwishoni mwa wiki, zimedhihirisha kuwa ukweli wa mambo unadhihirika uwanjani

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Josephat Charo