Utekaji nyara wamalizika Algeria | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.01.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Utekaji nyara wamalizika Algeria

Vikosi vya jeshi la Algeria vimevamia eneo la kisima cha gesi asilia jana jumamosi(19.01.2013) ili kufikisha mwisho mzozo uliosababisha vifo vya raia wa kigeni 23 na Waalgeria,saba na pia watekaji nyara wameuwawa.

epa03545840 Filipino overseas workers, who were sent home by their employer in Algeria but clarified that they were hundreds of kilometers away from a gas plant hostage crisis, arrive at the Manila international airport in Manila, Philippines 20 January 2013. Algeria's minister of telecommunications said on 20 January that he expected more bodies to be found, a day after the army launched a bloody assault on a remote gas plant where militants had held hundreds of workers captive. Algerian authorities had said that 23 captives and 32 terrorists had been killed in the In Amenas gas facility in the Sahara desert, after the military launched a final assault to end the four-day hostage standoff. EPA/ROLEX DELA PENA

Hawa ni mateka walioachwa huru Algeria

Mateka 21 wameuwawa wakati eneo hilo lilipokuwa limezingirwa , hali iliyotokana na watu wenye silaha wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda waliposhambulia kituo cha kukusanyia gesi asilia cha In Amenas ndani ya eneo la jangwa la sahara mapema alfajiri siku ya Jumatano, imesema wizara ya mambo ya ndani.

Wateka nyara 32 pia wameuwawa, na kikosi maalum cha jeshi la Algeria kilifanikiwa kuwaacha huru wafanyakazi 685 raia wa Algeria pamoja na wafanyakazi kutoka nchi za nje wapatao 107, taarifa hiyo imesema.

Two British hostages Peter, left, and Alan, right, (no family name available), are seen after being released, in a street of Ain Amenas, near the gas plant where they have been kidnapped by Islamic militants, Saturday, Jan. 19, 2013. Algeria's special forces stormed the natural gas complex in the middle of the Sahara desert in a final assault Saturday, killing 11 militants, but not before they in turn killed seven hostages, the state news agency reported.(Foto:Anis Belghoul/AP/dapd)

Mateka waliosalimika nchini Algeria

Raia wa kigeni wauwawa

Miongoni mwa wale waliouwawa kuna idadi ambayo haijulikani ya raia wa kigeni , ikiwa ni pamoja na wanaotoka Uingereza, Ufaransa, Romania na Marekani, na wengi bado hawajulikani waliko.

Kampuni ya uhasindisi kutoka Japan ya JGC Corp. imesema leo kuwa Wajapani 10 na wafanyakazi wengine saba wa kigeni bado hawajulikani waliko, lakini imethibitisha kuwa wafanyakazi 61 miongoni mwa 78 wako salama.

An Algerian military helicopter flies over Amenas city, south east of Algiers, where Islamist militants have been holding foreigners hostage, January 19, 2013. More than 20 foreigners were captive or missing inside a desert gas plant on Saturday, nearly two days after the Algerian army launched an assault to free them that saw many hostages killed. The standoff between the army and al Qaeda-linked gunmen - one of the biggest international hostage crises in decades - entered its fourth day, having thrust Saharan militancy to the top of the global agenda. REUTERS/Louafi Larbi (ALGERIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS ENERGY)

Helikopta ya jeshi ikiwa angani Algeria

Wateka nyara wakiongozwa na Mokhtar Belmokhtar raia wa Algeria , ambaye ni kamanda wa zamani wa kundi la al-Qaeda katika eneo la Afrika ya kaskazini , wamewauwa watu wawili katika basi, Muingereza na raia wa Algeria , kabla ya kuwakamata mamia ya wafanyakazi mateka wakati walipokishambulia kituo hicho cha gesi asilia.

Kundi la Belmokhtar la "Signatories in Blood", waliotia saini kwa damu limekuwa likidai kumalizwa kwa uingiliaji kati kijeshi wa Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika nchi jirani ya Mali.

Kiongozi huyo wa kundi hilo la wapiganaji ameonya katika matamshi aliyotoa na kutangazwa jana jumamosi kuwa ataripua kituo hicho cha kusafisha gesi iwapo jeshi litafika karibu na kituo hicho.

Katika matamshi yake yaliyotangazwa na shirika la habari la Mauritania,kamanda wa kikosi cha Al-Mulathameen , Abdul Rahman al-Nigeri kutoka Niger amesema siku ya Alhamis wakati jeshi la Algeria lilipozingira maeneo ya wapiganaji wake.

A member of the Algerian special forces, also known as the kouksoul, attends a training in Biskra, south of Algiers in this June 28, 2007 file photo. At least 22 foreign hostages were unaccounted for on January 18, 2013 and their al-Qaeda-linked captors threatened to attack other energy installations after Algerian forces stormed a desert gas complex to free hundreds of captives, resulting in dozens of deaths. With Western leaders clamouring for details of the assault they said Algeria had launched on Thursday without consulting them, a local source said the gas base was still surrounded by Algerian special forces and some hostages remained inside. REUTERS/ Louafi Larbi/Files (ALGERIA - Tags: POLITICS MILITARY CIVIL UNREST)

Mwanajeshi wa Algeria

Nigeri anasemekana kuwa kiongozi wa ngazi ya juu kwa kiongozi mkuu wa wateka nyara Belmokhtar. Katika shambulio la Jumamosi , jeshi la Algeria liliwakamata magaidi 11, na kundi hilo la kigaidi liliuwa mateka wao saba raia wa kigeni.

Mauzo ya nje hayakuathirika

Wakati huo huo Algeria haijapunguza mauzo yake ya nje ya gesi baada ya kuanza kwa mzozo huo wa utekaji nyara, wizara ya nishati ya nchi hiyo imesema.

epa03540765 An undated handout photograph released by the British Petroleum (BP) company on 16 January 2013 shows the gas facility in Amenas, some 1300 km southeast Algiers, Algeria. Reports on 17 January 2013 state 34 hostages were killed and 26 freed during an attack by the Algerian military on the site where Islamist gunmen were holding a group hostage, France Info radio reported. EPA/BP / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES

Kituo cha gesi kilichotekwa na wapiganaji Algeria

"Washirika wetu hawajaathirika kutokana na hali hiyo. Hatukupunguza mauzo yetu ya nje ya gesi, tumeweza tu kujaliza upungufu huo kwa uzalishaji kutoka katika maeneo mengine ya nchi, " shirika la habari la APS limemnukuu Youcef Yousfi.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe
Mhariri : Stumai George

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com