1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utawala wa kijeshi Guinea waamuru kuvunjwa kwa serikali

Amina Mjahid
20 Februari 2024

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeamuru kuvunjwa kwa serikali iliyokuwa madarakani tangu mwezi Julai mwaka 2022 bila kutoa sababu za uamuzi huo kuchukuliwa wala muda wa kutangazwa kwa serikali mpya.

https://p.dw.com/p/4cc5W

Hayo yameelezwa na msemaji wa utawala huo wa kijeshi Jenerali Amara Camara bila hata hivyo kutoa sababu za uamuzi huo wala kusema ni lini serikali mpya itakapotangazwa.

Jenerali Camara ameongeza kuwa kwa sasa shughuli za serikali zitasimamiwa na wakurugenzi wa baraza la mawaziri, makatibu wakuu na manaibu katibu hadi serikali mpya itakapoteuliwa. Guinea imekuwa ikiongozwa na jeshi tangu mapinduzi ya mwezi Septemba mwaka 2021.

Kiongozi wa zamani wa Kijeshi wa Guinea atoroshwa gerezani

Kufuatia shinikizo la kimataifa, kiongozi wa serikali hiyo ya kijeshi Kanali Mamady Doumbouya ameahidi kufanya mageuzi makubwa nchini humo na pia kuwa atarejesha utawala kwa viongozi wa kiraia watakaochaguliwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.