Utajiri wa Lugha ni Lahaja | Masuala ya Jamii | DW | 02.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Utajiri wa Lugha ni Lahaja

Kongamano la lugha ya Kiswahili hufanyika kila mwaka mjini Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Wataalamu wa lugha hualikwa kutoa mchango wao kuhusu jinsi lugha hii inavyoendelea kukua na kuangazia changamoto zilizoikabili.

Bayreuth - 28. Swahili Kolloquium

Mohammed Khelef (kulia) akimhoji Hassad Edward mjini Bayreuth

Miongoni mwa utajiri wa lugha ni lahaja zake zinazozungumzwa na watumiaji asili wa lugha hiyo kama kilivyo Kiswahili, lugha ya upwa wa Afrika Mashariki ambayo imesambaa kote Afrika Mashariki na hata ndani ya bara hilo.

Mohammed Khelef aliyehudhuria Kongamano la siku tatu la Kiswahili lililomalizika siku ya Jumanne (02.06.2015) mjini Bayreuth, kusini mwa Ujerumani, amekutana na mmoja wa wazungumzaji wa lahaja ya Kibajuni kutokea pwani ya Kenya, Hassan Edward. Na katika mazungumzo haya, Hassan anazungumzia tafauti zilizopo kati ya Kibajuni na lahaja nyengine za Kiswahili kwenye eneo hilo.

Kusikiliza mahojiano bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Mohammed Khelef
Mhariri:Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com