Urusi yailaumu Ukraine juu ya makubaliano ya kusitisha vita
9 Mei 2026
Matangazo
Likinukuu taarifa ya wizara hiyo ya ulinzi, shirika la habari la Interfax limeripoti kuwa vikosi vya Ukraine vilikuwa vimelenga maeneo ya kijeshi ya Urusi na miundombinu ya raia kwa kutumia droni na makombora.
Ripoti hiyo pia imesema mikoa ya Kaluga, Tula, Smolensk, Kursk, Bryansk na Belgorod nchini Urusi imeshambuliwa pamoja na Jamhuri ya Chechen na mikoa ya Stavropol na Krasnodar kusini mwa Urusi.
Hakukuwa na uthibitisho wa mashambulizi hayo kutoka upande wa Ukraine, lakini maafisa wake wakuu wameripoti mashambulizi 45 ya Urusi mapema leo katika eneo la Donbass mashariki mwa Ukraine.
Wizara ya ulinzi ya Urusi pia imeripoti mashambulizi 12 ya Ukraine. Hata hivyo taarifa za pande hizo mbili hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.