MigogoroUkraine
Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine kwa droni
13 Februari 2026
Matangazo
Urusi ilifyatua droni 154, limesema jeshi la anga la Ukraine na kuonya kuwa droni nyingine bado zingali kwenye anga la Ukraine.
Watu watatu na mvulana mmoja waliuliwa usiku wa jana katika jiji la Kramatorsk, zimesema mamlaka za eneo hilo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwenye hotuba yake ya jana jioni, alizitolea wito nchi washirika barani Ulaya kuharakisha utoaji wa mifumo ya ulinzi wa anga, akisema mashambulizi mapya ya makombora na droni kutoka Urusi yanaendelea kuhatarisha maisha ya raia na miundombinu muhimu nchini humo.