1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yawashambulia watu wanaoondolewa kwenye mafuriko

Daniel Gakuba
8 Juni 2023

Ukraine na Urusi zimetupiana lawama, kila upande ukiutuhumu mwingine kuwashambulia watu wanaoondolewa katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika mkoa wa Kherson.

https://p.dw.com/p/4SLXu
Mkazi wa Kakhovka akitumia boti wakati wa shughuli ya kuwahamisha wahanga wa mafuriko katika mkoa wa Kherson baada ya bwawa la Kakhovka kushambuliwa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametembelea eneo lililoathirika, na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia raia walio katika sehemu zinazokaliwa na Urusi.Picha: ALEKSEY FILIPPOV/AFP/Getty Images

Mafuriko hayo yalitokea baada ya bwawa la umeme la Kakhovka kuvunjwa katika mashambulizi ambayo nchi hizo pia zinashutumiana kuyafanya. Shughuli za uokozi zilianza bada ya miji na vijiji vilivyo karibu na mto Dnipro kuanza kufurika maji.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametembelea eneo lililoathirika, na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuwasaidia raia walio katika sehemu zinazokaliwa na Urusi. Mamia ya watu katika jimbo hilo hawana maji ya kunywa, hali iliyolilazimu jeshi la Ukraine kutumia ndege zisizo na rubani kuondosha maji ya chupa kwa watu wake walio na mahitaji. Hakuna upande huru uliothibitisha madai ya Urusi wala ya Ukraine.