1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wa Kenya waishutumu serikali kwa kuchochea matabaka

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameituhumu serikali ya nchi hiyo kuchochea vita kwa msingi wa matabaka.

https://p.dw.com/p/4PQZz
Kenia | Ausschreitungen und Proteste in Nairobi und Kisumi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Raila Odinga ametoa matamshi hayo kufuatia uvamizi wa genge la wahalifu katika shamba linalomilikiwa na familia ya rais wa zamani, Uhuru Kenyata, Jumatatu wiki hii. Kiwanda cha gesi kinachomilikiwa na familia ya Odinga pia kilishambuliwa siku hiyo, na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Rais William Ruto, kama ulipizaji kisasi kwa maandamano ya upinzani dhidi ya serikali. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliorushwa moja kwa moja katika kituo cha televisheni cha K24 chenye mafungamano na familia ya Kenyatta, Odinga alidai kuwa walichokitabiri wakati wa kampeni kuwa kambi ya Ruto ilikuwa ikiandaa vita vya kimatabaka kimedhihirika, na kuonya kuwa huo ni mwanzo wa kusambaratika. Licha ya mashambulizi hayo yaliyozilenga mali za familia yake na ya Kenyatta, Raila Odinga aliapa kuwa maandamano yataendelea kila Jumatatu na Alhamisi.