1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Uturuki wamtuhumu Erdogan kwa kuchochea vita

5 Januari 2022

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki Republican People's Party CHP, Kemal Kilicdaroglu, amemtuhumu Rais Recep Tayyip Erdogan kwa kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

https://p.dw.com/p/45Amj
Türkei Kemal Kilicdaroglu
Picha: Adem Altan/AFP

Kilicdaroglu ameyasema haya saa chache baada ya Rais Erdogan kusema kwamba atakabiliana na maandamano yoyote dhidi ya serikali yake.

Chama cha CHP na vyama vyengine vya upinzani vinataka kufanyike uchaguzi wa mapema nchini humo kutokana na mfumuko mkubwa wa bei na mgogoro wa sarafu ya lira.

soma zaidi: Tunisia: Mvutano mkubwa baada ya rais kulisimamisha bunge

Lakini chama tawala cha Kihafidhina cha Erdogan, AKP, na marafiki zake wa kizalendo wanasema uchaguzi utafanyika wakati uliopangiwa tu mwaka 2023. Uchaguzi mpya nchini Uturuki unaweza kuitishwa na rais au bunge tu.