1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Watu nusu milioni wakikimbia mapigano Kongo

24 Novemba 2023

Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Wakimbizi UNHCR imesema takriban watu nusu milioni wamekimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

https://p.dw.com/p/4ZQOM
Raia wa Kongo wakishuka katika lori la UNHCR baada ya kukimbia mapigano
Raia wa Kongo wakishuka katika lori la UNHCR baada ya kukimbia mapiganoPicha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Shirika hilo limesema watu 450,000 wameyakimbia mapigano huku 200,000 wakiwa ni wakimbizi wa ndani ambao kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa misaada ya kibinaadamu, na kwamba kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binaadamu ikiwa ni pamoja na ubakaji.

Soma pia:M23 wakiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Kongo

UNHCR imesema hali inazidi kuzorota katika mkoa wa Kivu Kaskazini unaopakana na mataifa ya Uganda na Rwanda na kwamba eneo hilo limekumbwa na mgogoro kwa muda mrefu. Vikosi vya serikali vinajaribu kuchukua udhibiti wa eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali.