Umoja wa Ulaya kuisaidia Mali kijeshi | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Umoja wa Ulaya kuisaidia Mali kijeshi

Umoja wa Ulaya unafanya mchakato wa kuanzisha jeshi la kuaminika nchini Mali, ambako waasi wenye itikadi kali ya Kiislamu wamelidhibiti eneo la kaskazini baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

African Union Chief Nkosazana Dlamini-Zuma (front L) and Mali's President Dioncounda Traore attend a high level international meeting in Bamako, October 19, 2012. Regional leaders joined international organisations in Bamako on Friday trying to narrow their differences over whether al Qaeda-linked Islamists in the north of Mali should be dislodged via military intervention or a more gradual political approach. REUTERS/Adama Diarra (MALI - Tags: POLITICS)

Mkutano wa viongozi wa Afrika kuhusu matatizo nchini Mali

Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Mauel Barroso, aliyezungumza akiwa pamoja na Rais Thomas Boni Yayi wa Benin, katika mkutano na waandishi habari kwa mara ya kwanza tangu kuwepo madai ya kupanga njama ya kumuua kwa kumpa dawa yenye sumu.

Barroso ambaye alikuwa Cote d'Ivoire, amesema viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaendelea kuwa makini sana na hali nchini Mali. Ameongeza kusema kuwa kwa sasa wanafanyia kazi mipango kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba kuna serikali na jeshi la kuaminika nchini Mali.

Germany's new Chancellor Angela Merkel, left, is welcomed by EU Commission President Jose Manuel Barosso upon her arrival at EU Commission headquarters in Brussels, Wednesday Nov. 23, 2005. (AP Photo/Geert Vanden Wijngaert)

Rais wa halmashauri ya umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso,(kulia) akiwa na kansela Merkel

Makundi yenye itikadi kali wakiwemo wanachama wa tawi la mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kaskazini mwa Afrika, wamelitwaa eneo la kaskazini la Mali huku kukiwa na machafuko yaliyotokana na mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka huu, ambayo yalifanywa na wanajeshi wa vyeo vya chini.

Serikali yashindwa

Hata hivyo, serikali ya mpito ya kiraia imeshindwa kujizatiti na serikali za mataifa ya Magharibi zinahofia kuwa eneo hilo linaweza kuwa makaazi ya wapiganaji wenye itikadi kali.

Der Präsident von Benin, Thomas Boni Yayi, spricht am Sonntag (04.11.2007) im Kloster Eberbach bei Eltville bei einer Pressekonferenz. Bundespräsident Köhler hatte zur dritten von ihm veranstaltete Afrika-Konferenz unter dem Titel Herausforderungen des Wandels - afrikanische und deutsche Antworten geladen. Foto: Frank Rumpenhorst dpa/lhe +++(c) dpa - Report+++

Rais wa Benin Thomas Boni Yayi

Viongozi wa Ulaya wameahidi kukiunga mkono kikosi cha jeshi cha Afrika ambacho kitapelekwa Mali kuwaondoa waasi hao, lakini wamesema msaada wao hautahusisha kupelekwa kwa wanajeshi wa Umoja wa Ulaya.

ECOWAS pia yataka kusaidia

Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi-ECOWAS, ambayo Benin ni mwanachama, imesema iko tayari kupeleka kikosi cha kijeshi nchini Mali, lakini sababu kadhaa zinachelewesha mpango wa kupelekwa kwa kikosi hicho.

(L-R) Benin's President Thomas Boni Yayi, Niger's President Mahamadou Issoufou and Guinea-Bissau interim President Serifo Nhamadjo attend a meeting of regional group Economic Community of West African States (ECOWAS) in Yamoussoukro June 29, 2012. REUTERS/Thierry Gouegnon (IVORY COAST - Tags: POLITICS)

Mkutano wa ECOWAS kuijadili Mali mjini Yamoussoukro

Rais Yayi ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amesema yeye na Barroso wamejadiliana kuhusu jukumu la Ulaya kwenye mzozo wa Mali, lakini hakuzungumzia chochote kuhusu njama za kutaka kumuua.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, mpwa wa Rais Yayi, daktari wake na wengine walipanga njama za kumuua kwa kumpa dawa za kutuliza maumivu zenye sumu.

Watu watatu wanaripotiwa kushikiliwa, huku vibali vya kuwakamata watuhumiwa wengine wawili vikiwa vimetolewa. Baadhi ya watu wanaasema kuwa madai hayo yalikuwa na lengo la kuwachafua maadui wa rais, akiwemo mtuhumiwa kinara wa kupanga njama hizo, mfanyabiashara Patrice Talon, ambaye alikuwa akimuunga mkono Rais Yayi kabla ya kuripotiwa kuhitalifiana na rais huyo kutokana na mzozo wa mikataba.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/AFPE

Mhariri: Sekione Kitojo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com