1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Umoja wa Mataifa waamuru Urusi iondoe vikosi vyake Ukraine

24 Februari 2023

Umoja wa Mataifa umepiga kura kwa wingi kuitaka Urusi kuwaondoa mara moja na bila masharti wanajeshi wake nchini Ukraine wakati vita hivyo vikitimiza mwaka mmoja na kutolewa mwito wa amani ya haki ya kudumu.

https://p.dw.com/p/4NvVq
UN-Generalversammlung zum Ukraine-Konflikt in New York
Picha: John Minchillo/AP/picture alliance

Ukraine imepata uungwaji mkono mkubwa katika kura isiofungamana na sheria ambayo ilishuhudia wanachama 141 kati ya 193 wa umoja huo wakiunga mkono, 7 wakipinga huku wanachama 32 ikiwemo China ambayo imeonekana kujenga uhusiano wa karibu na Kremlin haikushiriki zoezi hilo pamoja na India.

Mkuu wa sera za kigeni Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amesema kura hiyo ni ushahidi kwamba sio tu nchi za Magharibi pekee zinazoiunga mkono nchi yake, kutokana na uvamizi wa Urusi.

Licha ya uungwaji mkono wake kutoka kwenye nchi chache tu, Urusi imetumia uwezo wake wa kura ya turufu kuzuia hoja zozote za kisheria dhidi yake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.