1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yahofia mbinu mpya za mashambulizi ya Urusi

13 Mei 2026

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametahadharisha juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa mashambulizi ya droni za Urusi kwa siku nzima ya Jumatano.

https://p.dw.com/p/5DhMQ
Ukraine Kyiv 2026 | Volodymyr Zelensky akifanya mahojiano na AFP
Ukraine inahofia mbinu mpya ya Urusi ya kufanya mashambulizi nyakati za mchana badala ya usikuPicha: Genya Savilov/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mamia ya droni yalikuwa kwenye anga ya Ukraine wakati Moscow ikiwa imebadilisha mbinu na kushambulia zaidi nyakati za mchana.

Tangu vita hivyo vilipoanza miaka minne iliyopita Urusi imekuwa ikifanya mashambulizi makubwa majira ya usiku, lakini katika wiki za karibuni imefanya mashambulizi kama hayo mchana na kuvuruga pakubwa shughuli za wakaazi.

Hata hivyo, Urusi imekanusha kuwalenga kwa makusudi raia lakini tayari imewaua maelfu wakati wa vita, na kwa upande mwingine ikijipa uhalali wa kushambulia miundombinu ya raia, kama mbinu ya kudhoofisha uwezo wa Ukraine vitani.