1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Moscow yadai kukikamata kijiji kingine cha Donesk

25 Mei 2024

Urusi imesema hii leo kwamba imekikamata kijiji kingine huko Donesk, mashariki mwa Ukraine cha Arkhangelske.

https://p.dw.com/p/4gHRN
Ukraine | Mashambulizi kwenye mkoa wa Kharkiv
Kikosi cha zimamoto akiwa anazima moto baada ya Urusi kushambulia kiwanda cha uchapishaji huko Kharkiv, Ukraine Mei 23, 2024.Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Ukraine aidha imesema Moscow inazidisha mashambulizi yake nje ya mkoa wa Kharkiv, ulioko kaskazini mashariki mwa Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake wamechukua udhibiti wa kijiji cha Arkhangelske kinachopatikana kaskazini mwa mji wa Donetsk.

Kijiji hicho kidogo kilichopo kwenye uwanja wa vita kipo karibu na mji wa Ocheretyne ambao Urusi ilidai kuudhibiti mwezi uliopita.

Awali, Ukraine ilisema vikosi vyake vilizuia mashambulizi mawili katika eneo la Kharkiv na mapigano yalikuwa yanaendelea karibu na mji wa Vovchansk, ambao Moscow inajaribu pia kuuteka.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema jana kwamba alitembelea Kharkiv na kukutana na maafisa kujadiliana namna ya kulilinda eneo hilo na hasa mji wa Vovchansk.