Ujumbe wa UNAMID wapendekezwa kuondolewa Darfur | Matukio ya Afrika | DW | 14.11.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ujumbe wa UNAMID wapendekezwa kuondolewa Darfur

Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa Ijumaa wamependekeza kusimamisha mpango wao wa pamoja wa kutuma ujumbe wa askari wa kulinda amani jimbo la Darfur.

Viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa Ijumaa wamependekeza kusimamisha mpango wao wa pamoja wa kutuma ujumbe wa askari wa kulinda amani huko Darfur.

Pendekezo hilo limetolewa baada ya kushuhudiwa mabadiliko mazuri ya kisiasa nchini Sudan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mkuu wa Umoja wa Afrika Moussa Faki, walioiandika ripoti hiyo, wanakadiria kuwa kuondolewa kwa ujumbe huo kutoka Darfur kutachukua miezi sita, muda ambao pia utategemea jinsi Covid-19 na msimu wa mvua utakavyokuwa katika eneo hilo.

Soma zaidi: Idadi ya kikosi cha UNAMID kupunguzwa Darfur

"Tunapendekeza jumuiya ya kimataifa, haswa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na IGAD waendelee kuchunguza, pamoja na mamlaka ya Sudan, hatua zinazofaa za kusaidia kudumisha amani, usalama na juhudi za maendeleo," walisema viongozi hao.

New York António Guterres UN-Konferenz zu Frauenrechten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Askari wataanza kuondolewa Desemba 31

Katika ripoti yao ya pamoja iliyowasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jumuiya hizo mbili zimependekeza ujumbe wa askari wa kulinda amani ujulikanao kama UNAMID, uondolewe nchini Sudan kuanzia Desemba 31.

Ujumbe wa UNAMID, ambao ulianza operesheni zake nchini Sudan tangu 2007, unajumuisha walinda amani 8,000 ingawa wakati wa kilele chake idadi hiyo iliwahi kufika hadi askari 16,000.

Wakati huo huo bado hakujateuliwa kiongozi wa ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa ulioundwa mnamo mwezi Juni, kwa lengo la  kusaidia mabadiliko ya kisiasa ya Sudan kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais Omar al-Bashir mwaka jana.

Chanzo: afp

DW inapendekeza