1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Uingereza kuongoza majadiliano ya mpango wa amani wa Ukraine

25 Novemba 2025

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer hii leo anatarajiwa kuzungumza na washirika wa Ukraine wa Ulaya, kufuatia majadiliano ya mpango wa awali wa amani katika taifa hilo lililokumbwa na vita.

https://p.dw.com/p/54AFh
Uingereza London 2025 | Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akipeana mkono na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akipeana mkono na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, siku ya mkutano wa Muungano wa Walio Tayari, katika ofisi zake za Dwoning Street 10 jijini London, Uingereza, Oktoba 24, 2025Picha: Jaimi Joy/REUTERS

Starmer atawaongoza wakuu wenzake kwenye mazungumzo ya kile kinachotajwa "muungano wa walio tayari" baada ya majadiliano ya mwisho wa wiki kati ya Marekani na Kyiv ya kusuluhisha mgogoro na Urusi.

Starmer na viongozi wengine wa magharibi walimepinga mpango wa awali wa amani wa Rais Donald Trump wenye vipengele 28 kabla ya mazungumzo mjini Geneva, na kuibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa Ukraine kuachilia maeneo na kupunguza jeshi lake.

Kabla ya mazungumzo haya, Starmer alisema washirika wote katika muungano huo walikuwa wamejikita katika kufikia "amani ya haki na ya kudumu" nchini Ukraine.