1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda na hofu ya kutokea vurugu Kenya

Admin.WagnerD27 Februari 2013

Serikali ya Uganda nayo imekuwa ikijiandaa kuhakikisha kuwa wananchi wake hawataathirika kwa njia yoyote ile iwapo machafuko yatatokea nchini Kenya kama ilivyofanyika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.

https://p.dw.com/p/17mRH
Uganda's President Yoweri Museveni speaks during a press conference at his country home in Rwakitura, about 210 kilometres from the capital Kampala, on September 24, 2012. Museveni said he sent a team of legislators to the United Nations' headquarters in New York City to lobby for financial assistance for the neutral force that is to be based in the Democratic Republic of Congo to stabilize the country following unrest due to M23 rebels intending to oust the incumbent president Joseph Kabila. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI (Photo credit should read ISAAC KASAMANI/AFP/GettyImages)
Rais Yoweri Museveni wa UgandaPicha: AFP/Getty Images

Pamoja na kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki, rais Museveni ndiye rais ambaye amekuwa madarakani kwa muda mrefu na kulingana na desturi za kiafrika, ushauri wa wazee huwa jambo muhimu sana.

Uganda usafirisha bidhaa zake nyingi kupitia mipaka ya Kenya kama vile Busia na Malaba na ikiwa kutakuwa na machafuko yoyote nchini Kenya, Uganda bila shaka uathirika. Machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 nchini Kenya yalisababisha upungufu wa mafuta ya gari na bidhaa muhimu ambazo zilikwama kwenye bandari ya Mombasa.

Ahadi ya kukabiliana na tatizo la mafuta

Uganda wakati huo haikuwa imeweka akiba ya mafuta jambo lililoathiri sana usafiri. Sasa Rais Museveni anawahakikishia wananchi wake kuwa hilo halitatokea tena. "Ule wakati lilikuwa jambo la kushangaza na hatukua tunatarajia machafuko kutokea Kenya na ndio sababu tukapatikana tukiwa hatujajitayarisha. Ingawa hatutarajii shida zozote nchini Kenya, sasa hivi tumejitayarisha na ndio sababu tukaifungua barabara ya kusini ya kusafirisha bidhaa kupitia nchini Tanzania. Tumejiandaa sasa". Alisema rais Museveni.

Bandari ya Dar es Salaam, Tanzania
Bandari ya Dar es Salaam, TanzaniaPicha: DW /Maya Dreyer

Wafanyi biashara wa Uganda upendelea kusafirisha bidhaa zao kupitia nchini Kenya kwa sababu hiyo ndio njia fupi ukilinganisha na ile ya Tanzania. Ingawa rais Museveni anawaakikishia wananchi wake kuwa kufunguliwa kwa barabara ya kupitia Tanzania kutahakikisha kuwa hawakosi bidhaa wanazohitaji, wananchi wanahofia kuwa bei ya bidhaa hizi huenda ikapanda kwa sababu ya bei ghali ya usafirishaji wa bidhaa hizi kupitia Tanzania.

Bei ya dola imezidi kupanda

Tayari, bei ya dola imepanda. Mojawapo ya sababu zinazochangia ikiwa wafanyibiashara wanaziitaji dola sana wanunue bidhaa za kutosha ili kuhakikisha kuwa hawataathirika na lolote lile litakalotokea nchini Uganda.

Bei ya dola ikipana, mafuta nayo yanapanda. Kuanzia wiki jana, bei ya lita moja ya petroli imepanda kutoka 3600 pesa za uganda na kufikia shilingi 3,900 ambazo ni sawa na dola moja na nusu pesa za marekani.

Mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda alihudhuria kikao cha waandishi habari kilichoitishwa na rais Yoweri Museveni nyumbani mwake Rwakitura magharibi mwa Uganda na kututumia ripoti ifuatayo. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya kusikilizia masikioni hapo chini.

Mwandishi Leyla Ndinda
Mhariri Josephat Charo