Umewahi kusikia kuhusu ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa mwilini kitabibu ``Osteoporosis``?
Basi huo ni ugonjwa unaosababisha kulemaa kwa uthabiti wa mifupa kutokana na kupungua kwa madini ya `kalshiamu` na huifanya mifupa kuwa laini inayoweza kuvunjika kwa urahisi.
Ugonjwa huo huanza taratibu kwa miaka mingi na mara nyingi hugundulika pale ajali ndogo tu inaposababisha mifupa kuvunjika.