UEFA yaondoa vikwazo dhidi ya Man City, PSG | Michezo | DW | 04.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

UEFA yaondoa vikwazo dhidi ya Man City, PSG

Shirikisho la kandanda Ulaya – UEFA limeondoa vikwazo kadhaa lilivyoziwekea Manchester City na Paris Saint Germain kama sehemu ya sheria zake za haki katika masuala ya fedha miongoni mwa vilabu

UEFA imesema imeondoa baadhi ya vikwazo kuhusiana na shughuli za uhamisho wa wachezaji, gharama za wafanyakazi na idadi ya wachezaji wanaoshiriki katika mashindano ya vilabu vya UEFA ambavyo vilikuwa vimewekwa dhidi ya vilabu hivyo viwili mwaka jana.

Shirikisho hilo limesema hatua hiyo imefikiwa baada ya City na PSG kufikia baadhi ya malengo kuelekea katika kuzingaita sheria hizo za utaratibu wa haki za masuala ya kifedha. UEFA haikutoa maelezo zaidi kuhusiana na hilo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com