UEFA inaandaa mkutano mkuu Budapest | Michezo | DW | 02.05.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

UEFA inaandaa mkutano mkuu Budapest

Kamati kuu ya UEFA inakutana mjini Budapest katika mkesha wa mkutano mkuu wa Shirikisho hilo la Kandanda Ulaya lakini hatima ya rais wao aliyesimamishwa kazi Michel Platini itaighubika mikutano hiyo

Uongozi wa UEFA utajadili leo miundo ya mashindano, masuala ya kinidhamu na kusikiliza ripoti nyingine muda mfupi kabla ya kuanza dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 nchini Ufaransa kuanzia Juni 10.

UEFA inataka kudhihirisha kuwa ingali na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua maamuzi katika wakati huu ambapo kuna mgogoro wa uongozi, huku ikisubiri uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo kuhusu Platini. Platini alikata rufaa dhidi ya hatua ya FIFA kumsimamisha kazi na kesi hiyo ikasikilizwa Ijumaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu