1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya bunge la Somalia yaahirishwa hadi Novemba

6 Septemba 2021

Uchaguzi wa wabunge wa Somalia umeahirishwa na utafanyika tena Novemba, hatua ambayo itaathiri kuchaguliwa kwa rais.

https://p.dw.com/p/3zyBr
Somalia Mogadischu Parlament
Picha: STRINGER/AFP/Getty Images

Kura ya wabunge ilikuwa inastahili kufanyika wiki hii pamoja na kuchaguliwa kwa spika kisha kuapishwa kwa wabunge hao kufanyike wiki ijayo ili waweze kumchagua rais mnamo Oktoba 10.

Ila tume ya utekelezaji wa uchaguzi imeandika ratiba mpya kwa ajili ya mchakato huo ambao sasa utafanyika kati ya Oktoba mosi na Novemba 20.

soma zaidi:Bunge la Somalia labatilisha nyongeza ya muhula wa Rais

Ratiba hiyo iliyoonekana na shirika la habari la Reuters haikutoa tarehe kamili ambayo wabunge watamchagua rais.

Muhula wa serikali iliyoko madarakani sasa uliisha mnamo mwezi Februari.