TUTUMIE VIDEO YA KOMBE LA DUNIA! | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 24.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

TUTUMIE VIDEO YA KOMBE LA DUNIA!

Jee, unataka kuwa sehemu ya mradi wa kipekee wa Televisheni? Kuwa mpiga picha wetu!

Basi chukua Kamera yako, Tablet au Smartphone na utupigie picha ya video ya watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia mnamo Julai 13. Video yako huenda ikawa sehemu ya makala maalum ya Deutsche Welle itakayorushwa hewani mnamo Julai 17.

NANI?
Haijalishi kama mko watu thelathini kwenye baa mtu mmoja kwenye meli ya mizigo, au hata wawili tu ndani ya chumba cha kulala. Jee, unawafahamu watu wachangamfu, wenye kufurahisha na sehemu za kuvutia? Labda marafiki zako? Kazini? Au labda sehemu fulani karibu na unakoishi mtaani kwako? Tunatafuta video ya kipekee na ya kuvutia zaidi.

TUNACHOJITAJI
Picha yenyewe: iweke kamera yako chini au juu ya televisheni na urekodi namna mashabiki watakavyoitazama fainali hiyo kwa dakika 90 – furaha, wasiwasi, hofu, kukata tamaa, vifijo na shangwe! Video hii ya kipekee itaonyeshwa kila wakati kwenye makala yetu ya televisheni: Wakati ulimwengu ukitazama televisheni, televisheni inautazama ulimwengu! Picha za nje ya eneo utakalokuwa pamoja na mawazo mengine yenye ubunifu yanakaribishwa hata zaidi.

MUDA
Video ya dakika 3 itafaa zaidi.

LINI?
Tunahitaji cideo zako katika kipindi cha saa 24 baada ya mechi ya fainali kukamilika. (Julai 14, 10 pm GMT)

TUTAPATAJE?
1. Tuma video zako kwa kutumia WeTransfer au Dropbox. Anwani yetu ni: worldcup@dw.de au
2. Weka video zako kwenye YouTube au Vimeo na kisha ututumie link yako: worldcup@dw.de
Tafadhali tujulishe mji na nchi yako, ili tuweze kuandika kwenye televisheni.

Kuwa sehemu ya mradi wa kipekee! Tunasubiri kuona video zako za Kombe la Dunia!

Kama una maswali, tafadhali wasiliana nasi

barua pepe: worldcup@dw.de
Facebook: facebook.com/dw.kickoff
Twitter: twitter.com/dw_sports

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com