1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuchel kuisusa mechi inayoweza kuipa taji Leverkusen

12 Aprili 2024

Kocha wa klabu ya soka ya Bayern Munich Thomas Tuchel amesema hatoitizama mechi ambayo yumkini itaiwezesha klabu pinzani ya Bayer Leverkusen kutangazwa mabingwa wa msimu huu wa ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga

https://p.dw.com/p/4ehn4
Thomas Tuchel
Kocha wa klabu ya soka ya Bayern Munich Thomas TuchelPicha: Martin Sylvest/AP Photo/picture alliance

Leverkusen itateremka dimbani kupimana ubavu na Werder Bremen, kwa mchezo utakaoamua iwapo vijana hao wa kocha Xabi Alonso wataandika historia ya kutwaa taji la Bundesliga na kumaliza utemi wa Bayern Munich waliolinyakua taji hilo kwa miaka 11 mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa bahari mjini Munich, Tuchel amesema haitoutizama mchezo huo na badala yake atasubiri mechi kati ya timu yake na Arsenal wiki ijayo kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya.

Tuchel: Tuko pazuri kuelekea mechi za kimataifa

Leverkusen ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza msimu wa ligi watatawazwa washindi wa Bundesliga kama watafanikiwa kupata alama 3 kwenye mchezo wake na Bremen.