Tripoli yazidi kushambuliwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tripoli yazidi kushambuliwa

Milipuko mikubwa imesikika mfululizo, mapema leo katika mji mkuu wa Libya Tripoli, uliongome ya kijeshi ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

default

Mji wa Tripoli washambuliwa zaidi

Milipuko 13, ilisikika jana usiku na mapema leo asubuhi. Hata hivyo haikuelezwa mara moja nini lengo la milipuko hiyo.

Lakini kituo cha Televisheni cha taifa cha Al Jamahiriya kimeripoti kwamba Majeshi ya NATO yameshambulia maeneo ya raia na yale ya kijeshi katika maeneo ya Ain Zara na Tajoura, mashariki ya Tripoli.

Tripolis Gaddafi Libyen Luftangriff NATO

Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa

Kituo hicho, kilinukuu duru za kijeshi, kwa kusema kuwa kuna watu walioathiriwa na mashambulio hayo, lakini hakikutoa taarifa kamili.Wakati huohuo waasi 10 wa Libya wameripotiwa kuuawa na wengine 172 wamejeruhiwa katika shambulio lililofanywa jana katika mji wa magharibi mwa nchi hiyo wa Brega, wakati waasi hao wakiendelea mbele na mapambano kwa kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Gaddafi.

DW inapendekeza

 • Tarehe 17.07.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11wpu
 • Tarehe 17.07.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza(ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11wpu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com