Tour de France | Michezo | DW | 26.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Tour de France

Mbio za baiskeli za Tour de France zimeingia mashakani.zimegubikwa na kashfa za doping -madhambi ya kutumia madawa kutunisha misuli n a kutia kasi.Nini hatima ya mbio hizi ?

Michael Rasmussen ambaye ameangushwa kutoka mashindano ya Tour de France

Michael Rasmussen ambaye ameangushwa kutoka mashindano ya Tour de France

Mbio za baiskeli za mwaka huu Tour de France-zaonesha zaongoza kaburini .Kashfa zake za madhambi ya doping kila kukicha zazidi kukirihisha.

Jana,aliekua akiongoza mbio hizo hadi sasa Michael Rasmussen wa Danmark,alitiwa munda na wafadhili wake kutoka holland-RABOBANK na ameangushwa kabla kumaliza mbio hizo.

Rasmussen,masaa machache kabla,alishinda hatua ya mwisho kwenye milima ya Pyrenäen na akivaa fulana ya manjano,ikionekana hakuna wa kumzuwia kuwasili Paris,kama mshindi isipokua mfadhili wake Rabobank.

Inadhihirika sasa kuwa mbio za baiskeli za tour de France-mbio za mabingwa wa dunia zimefikia mfundoni ikiwa si ukingoni mwa kaburi kuzikwa.Zimegeuka kashfa tupu na fujo tupu.

Muendeshaji baiskeli pekee alietumainiwa kutawazwa bingwa mara hii –mshindi wa hatua mbili za mbio hizi Alexander Winkurow kutoka kasakhstan aligunduliwa na madhambi ya doping akiwa amejiiimarisha kwa damuisio yake.Bingwa wa zamani wa Itali Christian Moreni,akafumaniwa madhambi ya doping kwa dawa ya testosteron.Alievaa hadi jana jazi ya manjano Michael Rasmussen,mdanmark alitimuliwa nje na wafadhili wake Rabobank.Hata timu za akina Moreni na Winokurow zimejitoa safarini.

Subira ya mashabiki wa mbio za baiskeli haipo tena na Rasmussen na timu yake wametambua jana.

Kwa kutiwa munda kwa Rasmussen,mspain Alberto Contador,amepokea yeyxe jazi ya manjano kutoka kwa Rasmussen,lakini hata jazi yake yeye si safi.Kuna nyaraka zinazoonersha dhahiri-shahiri

Kuwa Contador alikua mteja wa daktari wa kispain,maarufu kwa madhambi ya doping Fuentes.Halafu kama miujiza jina lake likatolewa katika orodha ya watiliwa shaka madham,bi ya doping.

Mbio za baiskeli za tour de France zilisusiwa kuooneshwa na kutangazwa na vituo viwili vya TV vya Ujerumani ARD na ZDF pale ilipofichuka kwamba hata mjerumani Peter Sinkewitz,amefumaniwa na madhambi hayo ya doping na kuiabisha upya T-Mobile-wafadhili wake wa Ujerumani.

Kulifanyika mfano wa maandamano kupinga visa vya doping baadhi yawaendeshaji baiskeli waliposimaisha mbio kwa dakika chache.mmoja wa waendeshaji alikuwa Marcus Burghardt wa T-Mobile:

„Nina umri wa miaka 24 na nina azma ya kukimbia mbio za baiskeli kwa miaka 10 hadi 11 ijayo tena bila kutumia madawa.Lakini, kinachopita sasa,nina shakashaka kweli, iwapo mbio za baiskeli zina mustakbala mwema.“

Kwahivyo, mbio za baiskeli za tour de France ,zimegeuka mbio za kuelekea kaburini na siku zahesabiwa lini kuziambia buriani.Wafadhili wakubwa wa mbio hizi wanazingatia iwapo wajitoe kabisa ili wasichafue zaidi majina yao.

Labda ingelikua busara baada ya kisa cha jana cha Michael Rasmussen aliedanganya kwamba akijiandaa kwa mbio hizo huko Mexico,lakini ka kweli alikua Itali,zingevunjwa kabisa alao kwa mwaka huu.Ikiwa ufagio wa chuma hautapitishwa kusafisha madhambi ya doping katika Tour de France,basi kuna hatari mchezo huu mzima wa kispoti kuingia hatarini ikiwa si kaburini.

 • Tarehe 26.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbZ
 • Tarehe 26.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbZ