Tokyo kuandaa Michezo ya Olimpiki 2020 | Michezo | DW | 09.09.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Tokyo kuandaa Michezo ya Olimpiki 2020

Japan imeonja ushindi wa kinyang'anyiro cha kuandaa Michezo ya Olimpiki mwaka wa 2020, ikitarajia kuimarika uchumi wake baada ya miongo miwili ya kudorora kutokana na athari za tetemeko la ardhi Tsunami.

An aerial view shows people sitting in formation to the words thank you and displaying signs that collectively read Arigato (Thank You) during an event celebrating Tokyo being chosen to host the 2020 Olympic Games, at Tokyo Metropolitan Government Building in Tokyo, in this photo taken by Kyodo September 8, 2013. Tokyo was awarded the 2020 summer Olympic Games on Saturday, beating Istanbul in a head-to-head vote after Japanese Prime Minister Shinzo Abe delivered a charismatic plea to the International Olympic Committee and promised Japan's crippled nuclear plant was under control. MANDATORY CREDIT. REUTERS/Kyodo (JAPAN - Tags: SPORT OLYMPICS POLITICS) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. MANDATORY CREDIT. JAPAN OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN JAPAN. YES

Tokio Japan Olympia 2020

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alijihusisha moja kwa moja katika juhudi za kuufanya mji wa Tokyo kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Olimpiki, na sasa anafahamu kibarua kilichopo cha kujiandaa kikamilifu kwa tamasha hilo. Abe amesema "Tungependa kuwashukuru wale wote waliouunga mkono mji huu. Wacha nimsalimu kila mtu aliyefanya juu chini katika kinyang'anyiro hiki, kama vile Uhispania na Uturuki. Kimekuwa kinyang'anyiro kirefu na kigumu na ningependa kuwapongeza wanamichezo wote pamoja na Gavana wa Tokyo na wanariadha, kwa kusaidia katika juhudi za kuandaa Michezo ya Olimpiki. Bila juhudi zao hatungelishinda ombi hili. Sasa, kazi halisi inaanza. Tutaanza maandalizi, kwa Michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu jijini Tokyo 2020 ili iwe yenye mafanikio".

Mchezo wa mieleka umefanyiwa mageuzi makubwa

Mchezo wa mieleka umefanyiwa mageuzi makubwa

Rais wa timu za Michezo ya Olimpiki ya Ujerumani na ambaye ni mgombea wa wadhifa wa Urais wa Kamati ya Olimpiki Duniani IOC Thomas Bach, anaelezea sababu zilizochangia kuchaguliwa mji wa Tokyo kama mwenyeji wa Mashindano ya Olimpiki 2020."Tokyo , kwa mtazamo wa wanachama wa IOC, katika hali hii tete ya dunia, inaangaliwa kama mahala salama,kwa kuzingatiwa pia desturi fulani za kutoa maombi. Wameboresha tena maombi yaao tangu walipoyatuma. Wanadhaamini utulivu upande wa fedha na pia upande wa kisiasa.Nnaamini hoja zote hizo zimechangia kuiona hatimae Tokyo ikiangaliwa kama mahala tulivu na salama kuliko kote kwengine."

Mieleka itakuwa sehemu ya michezo ya 2020

Na tukibakia huko Tokyo ni kwamba, kama wewe ni mpenzi wa mchezo wa mieleka, au kama wewe ni mwanamieleka, basi una sababu ya kuanza kujiandaa, kwa sababu mchezo huo umeongezwa katika orodha ya michezo itakayoshirikishwa katika mashindano ya Olimpiki mwkaa wa 2020 na 2024. Mchezo wa Mieleka ulipigiwa kura na kuishinda michezo ya baseball na squash baada ya mchezo huo wa jadi kufanyiwa mageuzi makubwa tangu ulipoondolewa kwa muda mwezi Februari. Mchezo wa mieleka ulipata kura 49 miongoni mwa wanachama 95 wa Kamati ya Kimataifa ya Ompiki – IOC.

Rais wa Kamati ya Maamuzi katika spoti FILA, Nenad Lalovic amesema mieleka siyo mchezo mpya, lakini mara hii wanaleta aina mpya ya mieleka. Kwamba wamejaribu kuuimarisha mchezo huo na kuufanya kuwa wa kuburudisha na kuwasisimua zaidi mashabiki. Kamati ya Michezo ya Olimpiki iliongeza Rugby na Gofu kwenye mashindano ya mwak wa 2016 mjini Rio. Michezo hiyo pamoja na Mieleka sasa inafikisha 28 jumla ya michezo katika mashindano ya Olimpiki.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/AFP/DPA

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman