Timu za Bundesliga kukumbana na za Premier League katika Champions League | Michezo | DW | 17.12.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Timu za Bundesliga kukumbana na za Premier League katika Champions League

Timu  tatu  za  Ujerumani  Bayern Munich, Borussia Dortmund kuoneshana  na Schalke 04 kuoneshana kazi  na  timu  za  England  katika Champions  League.

Upangaji  wa  timu katika  Champions  League katika  duru  ya   mtoano  ya timu  16 mchana  wa  leo  mjini  Nyon, Uswisi, umekamilika  na ni kwamba  timu  tatu  za  Ujerumani  zinapambana  na  timu  tatu  za Uingereza.  Schalke 04  ya  Ujerumani  itakwaana  na  Manchester  City  ya Uingereza.

Champions League FC Liverpool - SSC Neapel Klopp (Action Images via Reuters)

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool , timu yake inapambana dhidi ya Bayern Munich

Tottenham  Hotspurs ya  Uingereza  itajishughulisha  na Borussia  Dortmund ya  Ujerumani, na  Jurgen Klopp anawakaribisha Wajerumani  wenzake kutoka  katika  Bundesliga, Bayern Munich uwanjani  Anfield.

Atletico  Madrid  ya  Uhispania  inapambana  na Juventus  Turin  ya  Italia, wakati Manchester  United  itapimana  nguvu  na Paris saint-Germain  ya  Ufaransa.  Lyon  ya  Ufaransa  ina  miadi  na Barcelona  ya  Uhispania. Roma  ya  Italia  itatiana  kifuani  na  Porto  ya Ureno  na  Ajax  kutoka  Uholanzi  inakutana  na  miamba  ya  Uhispania Real  Madrid  mabingwa  watetezi.

Fußball Champions League - Liverpool vs Neapel | Mohamed Salah (Reuters/J. Super)

Mshambuliaji hatari wa Liverpool Mohamed Salah wa Liverpool

Kwa upade wa michuano  ya  mtoano  ya Europa League , mabingwa  mara tano wa  kinyang'anyiro  hicho Seville watapambana  na  Lazio  ya  Italia katika  duru  ya  timu  32. Valencia wanakibarua  dhidi  ya  mabingwa  wa zamani wa Ulaya  Celtic, Villarreal  wataoneshana  kazi  na  Sporting  na Betis wanakutana  na  Rennes ya  Ufaransa. Eintracht Frankfurt  ya Ujerumani  itaumana  na Shakhtar Donetsk, Arsenal inakwaana  na  BATE Borisov ya  Belarus, wakati  Chelsea  inamiadi  na  Malmo ya  Sweden.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo  / rtre / afpe / ape

Mhariri:  Iddi Ssessanga