Tiba ya Ebola ya China yawasili Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Tiba ya Ebola ya China yawasili Afrika

Watengeneza madawa wa China kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo wamepeleka madawa ya majaribio ya kutibu Ebola barani Afrika.Tiba hiyo ni kwa ajili ya wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya taifa hilo.

Ebola Opfer Angehörige 10.10.2014 Liberia

Wahudumu wa afya Liberia

Pamoja na jitihada hizo vilevile wanapanga kujenga vituo vya matibabu vya majaribio. Afisa mwendeshaji mkuu wa kampuni iliyotengeneza madawa hayo, Sihuan Pharmaceutical Holding Group Ltd, Jia Zhongxin amesema tayari wamekwisa safarisha maelfu kadhaa ya dozi za madawa aina ya JK-05 katika maeneo yaliathirika na kwamba kiasi kingine zaidi kitapelekwa pale kitakapohitajika.

Mripuko wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi, ambao unaelezwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000.

Jitahada za kimataifa

Ebola Screening Heathrow London Großbritannien 14.10.

Abiria katika uwanja wa ndege wa London

Serikali na makampuni ya kutengenea madawa duniani kote yamekuwa katika harakati za kutafuta tiba ya ugonjwa huo, ambao umesambaa katika maeneo ya mbali kama Marekani na Ulaya. Rais wa Marekani, Barack Obama ameahidi kufanya jitihada zaidi dhidi ya ugonjwa huo.

Meneja msaidi wa kampuni iliyotengeneza madawa hayo, Huo Caixia amesema wafanyakazi wa mashriki ya misaada wa Kichinia, wamekwisha chukua madawa hayo ili waweze kujikinga pale yanapotokea maambukizi miongoni mwao.

Kampuni hiyo iliyotengeneza madawa hayo, ambayo kwa sehemu fulani inamilikiwa na benki moja ya uwekezaji ya Marekani inatumaini kwamba dawa hiyo inaweza kuharakisha katika kuingia katika mzunguko wa matumizi ya raia nchini China.

Tayari imeingia katika makubaliano na chuo cha kutengeneza madawa cha kijeshi cha China, taasisi ya utafiti, ili dawa hiyo iweze kuthibitisha kwa ajili ya matumizi ya taifa hilo na kuingiza kabisa katika soko. Mpaka sasa madawa hayo yamethibitisha kwa matumizi ya dharura ya kijeshi tu.

Kama madawa haya yatadhirika kutibu itakuwa sifa kubwa katika sekta ya utengenezaji madawa nchini China na kutanua nguvu ya China barani Afrika kujiungezea umuhimu wake katika matiafa ya Afrika kama taifa la pili lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani.

Katika hatua nyingine jumamosi ijayo Ufaransa itaanza kufanya uchunguzi wa watu wenye maambukizi ya Ebola kwa wasafiri wote, wanaotokea Guinea kwa usafiri wa anga. Waziri wa Afya wa taifa hilo Marisol Touraine amesema maafisa wa afya watawapima viwango vya joto kwa abiria wote wanaotoka Conakry. Hatua hiyo ya Ufaransa inafutia ile iliyochukuliwa na mataifa mengine kama Uingereza, Canada na Marekani pamoja na kutoridhiwa na shirika la Afya Duniani WHO na Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Ulaya CDC.

Kwa muendelezo wa hatua hiyo leo hii mawaziri wa Afya wa Umoja wa Ulaya wanajiandaa kujadili namna ya kuanzisha uchunguzi wa watu wenye maambukizi ya Ebola katika viwanja vyote vya ndege barani Ulaya.

Na mripuko huo wa Ebola unaelezwa kuongeza zaidi kadhia ya baa la njaa katika mataifa yalioathiriwa barani Afrika. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema linapswa kuwafikia watu milioni 1.3 walio katika maeneo ya vijijini Liberia, Sierra Leone na Guinea.

Mwandishi: Sudi Mnette APE/RTR/DPA
Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com