1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi Taiwan lawaua watu 7 na kuwajeruhi 700

3 Aprili 2024

Tetemeko kubwa zaidi la ardhi kuwahi kuikumba Taiwan katika kipindi cha miongo miwili, limesababisha vifo vya watu 7 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 700 huku watu 77 wakiripotiwa kunaswa katika majengo yaliyoporomoka.

https://p.dw.com/p/4eNW4
Tetemeko la ardhi-Taiwan
Sehemu ya uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi huko TaiwanPicha: AFP

Tetemeko kubwa zaidi la ardhi kuwahi kuikumba Taiwan katika kipindi cha kama miongo miwili na nusu leo, limesababisha vifo vya watu watu 7 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 700 huku watu 77 wakiripotiwa kunaswa katika majengo yaliyoporomoka.

Ripoti zinaarifu kwamba waokoaji wanatumia ngazi kuwaokoa watu na kuwapeleka maeneo salama. Picha za televisheni zinaonyesha majengo yaliyopinda katika kaunti ya mashariki ya Hualien yenye milima na idadi ndogo ya watu, karibu na chimbuko la tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya richter.Tokyo yakumbwa na tetemeko la ardhi japo mamlaka haijatoa onyo la kutokea Tsumani

Tetemeko hilo limetokea wakati watu walipokuwa wakielekea makazini na wanafunzi shuleni na kusababisha tahadhari ya tsunami kutolewa katika pwani za kusini mwa Japan na Ufilipino. Tahadhari hiyo iliondolewa baadaye.