1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Tetemeko la 7.4 Indonesia latishia tsunami, mawimbi hatari

2 Aprili 2026

Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.

https://p.dw.com/p/5BY72
Mnato | Indonesia: Unajiandaje kwa tetemeko kubwa la ardhi?
Indonesia imekuwa ikikumbwa na matetemeko ya ardhi ambayo wakati mwingine pia husababisha tsunamiPicha: Iryanda Mardanuz/DW

Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 limetokea katika Bahari ya Molucca kaskazini mwa Indonesia, karibu na kisiwa cha Ternate, kulingana na Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani.

Tetemeko hilo lilisababisha tahadhari ya tsunami kutolewa kwa maeneo ya Indonesia pamoja na nchi jirani za Ufilipino na Malaysia.

Hakuna taarifa za mara moja kuhusu majeruhi, lakini mitetemeko midogo ya baadae yenye ukubwa hadi 5 imeripotiwa.

Mamlaka za Indonesia zimeitaka baadhi ya miji, ikiwemo Ternate na Tidore, kujiandaa kwa uwezekano wa uokoaji wa dharura, huku baadhi ya majengo yakiripotiwa kuharibika.

Tetemeko hilo lilitokea katika kina cha takribani kilomita 35 na kitovu chake kikiwa karibu kilomita 120 kutoka Ternate.

Maafisa wa tahadhari ya tsunami wamesema mawimbi hatari yanaweza kutokea ndani ya umbali wa kilomita 1,000 kutoka eneo la tukio.