1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Williams aongeza muda wa kuaga michuano ya US Open

31 Agosti 2022

Katika kile kinachotarajiwa kuwa mashindano yake ya mwisho kabisa, mshindi huyo mara 23 alishinda kwa seti za moja kwa moja dhidi ya Danka Kovinic.

https://p.dw.com/p/4GHNs
US Open Tennis Serena Williams
Picha: Charles Krupa/AP Photo/picture alliance

Williams alitangaza mapema mwezi huu kwamba mwisho wake wa kucheza tenisi unakaribia.

Taaluma ya tenisi ya Serena Williams inatarajiwa kudumu angalau siku mbili zaidi baada ya kumshinda mpinzani wake wa raundi ya kwanza katika mashindano ya US Open, Danka Kovinic, seti 6-3, 6-3.

Uwanja wa Arthur Ashe uliojaa watu ulishangilia kipenzi cha nyumbani, huku kukiwa na salamu za furaha kila pointi aliyoshinda, huku makofi ya heshima yakitolewa kwa mpinzani wake, akishika nafasi ya 80 duniani.

Ang'ara uwanjani

US Open Tennis Serena Williams
Serena WilliamsPicha: John Minchillo/AP Photo/picture alliance

Akiwa amevalia mavazi ya kung'aa yanayofaa katika hafla hiyo, Williams alitambulishwa kwa umati wa watu mjini New York kama Malkia wa Malkia, akimaanisha eneo ambalo US Open inafanyika, pamoja na utawala wake juu ya mchezo huo kwa robo karne.

Williams alianza vibaya, ikiwa ni pamoja na makosa mawili katika mchezo wake wa ufunguzi, kabla ya kutulia na kuchukua faida ya mapema na kuongoza 2-0.

US Open Tennis Serena Williams
Picha: Charles Krupa/AP Photo/picture alliance

Lakini alirejelea makosa mawili katika mchezo wa tatu, Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alipata tena faida ya kuchukua uongozi wa seti 5-3.

"Ninajisikia vizuri sana katika uga huu na mbele ya kila mtu hapa," williams alisema baada ya ushindi.

"Umati ulijawa na bashasha walinisaidia sana kujitahidi zaidi. Nilipata msukumo sana," aliongeza Williams, ambaye alishinda taji lake la kwanza kati ya mataji 23 makubwa katika uwanja huo huo mwaka 1999 alipokuwa na umri wa miaka 17.

Mapema mwezi huu, Williams alisema anajiandaa kumaliza kazi yake ya tenisi, lakini ushindi jumatatu usiku unaongeza muda wake wa kucheza kwa angalau mechi moja zaidi. Katika mechi ya mzunguko wa pili atacheza dhidi ya Anett Kontaveit wa Estonia.

 

https://p.dw.com/p/4GCF2