1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serana Williams atinga robo fainali US Open

2 Septemba 2013

Bingwa mtetezi wa mashindano ya US Open kwa upande wa wanawake Serana Williams (pichani juu) ameingia katika robo fainali ya mashindano hayo, kwa kumshinda Sloane Stephens kwa seti 6-4, 6-1.

https://p.dw.com/p/19aNp
Serena Williams of the U.S. hits a return to Maria Sharapova of Russia during their women's singles final match at the French Open tennis tournament at the Roland Garros stadium in Paris June 8, 2013. REUTERS/Stephane Mahe (FRANCE - Tags: SPORT TENNIS TPX IMAGES OF THE DAY)
French Open Finale 2013 Serena WilliamsPicha: Reuters

Williams sasa atakutana na mchezaji namabri 18 duniani Carla Suarez Navarro kutoka Uhispania, ambaye alimshinda mchezaji nambari 8 Angelique Kerber wa Ujerumani kwa seti 4-6, 6-3 na 7-6. "Ubora wa tenesi ulikuwa wa juu sana, Sloane ni mchezaji mzuri sana, na nilihisi hivyo lakini mwisho wa siku ilikuwa mechi ya raundi ya nne na bila shaka ni hisia za robo fainali kuliko nusu fainali," aliseam Williams baada ya mchezo huo wa raundi ya tatu.

Kwa upande wa wanaume, mshiriki wa mwisho kati ya 15 wa Marekani alipoteza, wakati Tim Smyczek, ambaye ni nambari 109 kwa ubora duniani alipopigwa kwa seti 6-4, 4-6, 0-6, 6-3 na 7-5 na Marcel Granollers kutoka Uhispania. Hiyo iliyafanya mashindano ya mwaka huu kuwa ya kwanza katika historia, kutokuwa na mwanaume hata mmoja kutoka nchi muandaji katika raundi ya nne.

Andy Murray
Andy MurrayPicha: Reuters

Granollers ambaye anashika nambari 43 duniani, atakutana na mchezaji nambari moja duniani Novak Djokovic. Bingwa mtetezi Andy Murray, bingwa wa US Open wa mwaka 2001, Lleyton Hewitt, mchezaji nambari 5 Tomas Berdych, Nambari 9 Stanislas Wawrinka na nambari 21 Mikhail Youzhny pia walifanikiwa kusonga mbele.

Jean Todt, rais wa shirika linaloongoza mchezo wa mbio za magari duniani FIA, atakabiliwa na upinzani kwa urais wake mwezi Desemba, baada ya Mkurugenzi mkuu wa shirika huru la hisani la Taasisi ya FIA David Ward, kujiuzulu nafasi yake baada ya miaka 12, ili apambane dhidi ya Todt. Ward mwenye umri wa miaka 56, alisema kipindi cha uchaguzi kinaanza mwezi huu wa Septemba, na kwa hivyo ilikuwa muhimu kwake kuwafikia wanachama wa FIA ili aweze kupata uteuzi.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/ape, ap, afpe, rtre
Mhariri: Josephat Nyiro Charo