TBILISI : Hali ni wasi wasi lakini shwari | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBILISI : Hali ni wasi wasi lakini shwari

Mji mkuu wa Georgia Tbilisi inaripotiwa kuwa uko katika hali ya wasi wasi lakini shwari baada ya Rais Mikhail Saakashvili kutangaza hali ya hatari nchi nzima hapo jana.

Saakashvili amechukuwa hatua hiyo kufuatia wiki nzima ya maandamano dhidi ya utawala wake akidai kwamba vikosi vya usalama vilikuwa na habari kwamba kuna mpango wa mapinduzi unaoungwa mkono na Urusi.Msemaji wa Ikulu ya Urusi amekanusha madai hayo.

Wizara ya Afya imesema zaidi ya watu 500 wamejeruhiwa hapo jana wakati vikosi vya usalama vilipotumia risasi za mpira na mabomu ya kutowa machozi kutawanya waandamanaji katika mji mkuu.

Waandamanaji wanamshutumu Saakashvili kwa kutumia vibaya madaraka yake na kwa sera za uchumi zilizoshindwa kuleta tija.

Chini ya utawala wa hali ya hatari shule na vyuo vikuu vitaendelea kufungwa hadi mwishoni mwa juma na televisheni ya taifa tu ndio itakyoruhusiwa kurusha matangazo yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com