Tanzania: Mkutano wa UKAWA na waandishi wa habari | Matukio ya Afrika | DW | 10.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Tanzania: Mkutano wa UKAWA na waandishi wa habari

Umoja wa katiba ya wananchi nchini Tanzania-UKAWA- uliolisusia Bunge maalum la katiba tokea mwezi Aprili, leo ulikuwa na mkutano na waandishi habari .

Wakuu wa vyama vya upinzani UKAWA

Wakuu wa vyama vya upinzani UKAWA

Madhumuni ya mkutano huo ni kueleza msimamo wa UKAWA kuhusu yalioafikiwa katika mazungumzo kati ya viongozi wa vyama vya kisiasa vinavyoundwa kile kinachojulikana kama Kituo cha Demokrasia Tanzania na Rais jakaya Kikwete kuhusu mkwamo uliojitokeza baada ya Ukawa kujitoa kwenye Bunge la katiba. Msimamo wa ukawa unafuatia maelezo yaliotolewa jana na Mwenyekiti wa Kituo hicho mbunge John Cheyo kuhusu matokeo ya mkutano wao na Rais Kikwe

Mohamed Abdul-Rahman amezungumza na katibu wa UKAWA Julius Mtatiro na kwanza anaelezea juu ya msimamo wao. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohamed Abdul-Rahman

Mhariri : Iddi Ssessanga

Sauti na Vidio Kuhusu Mada