1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban watu 45 wameuawa katika mapigano Somalia

10 Juni 2024

Polisi nchini Somalia imesema takriban watu 45 wameuawa na wengine 60 wamejeruhiwa kufuatia mapigano ya koo hasimu katikati mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4gqp4
Pressefreiheit Medienfreiheit in Afrika | Journalisten bei der Arbeit in Somalia
Picha: Mohamed Dahir/AFP/Getty Images

Afisa wa polisi wa jimbo la Galgadud, Ahmed Sahal amesema tukio hilo baya limehusisha wapiganaji kutoka katika koo za Marehan na Dir.

Mzozo huo ulitokea kwenye mji wa Landhere huko kaskazini ya Galgadud.

Kihistoria raia wa Somalia kwa idadi yao wamegawanywa katika koo na mara nyingi hujihusisha na migogoroya maeneo kwa ajili ya rasilimali na sababu za kisiasa.