1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Syriza

Syriza ni chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto nchini Ugiriki. Ndiyo chama kikubw azaidi katika bunge la nchi hiyo, na kiongozi wake Alexis Tsipras, ndiye waziri mkuu wa Ugiriki tangu Septemba 20, 2015.

Rangi rasmi za chama hicho ni nyekundu (ikiwakilisha siasa za mrengo wa kushoto), kijani (siasa za kijani) na zambarau (mavuguvugu ya kijamii). Chama cha Syriza kiliasisiwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2004, na mwaka 2015 kilipata nguvu iliyoweza kuvisambaratisha vyama vya jadi nchini Ugiriki, na kwa wakati huu ni chama kisicho na upinzani mkubwa nchini Ugiriki.