1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sumu yadaiwa kuuwa Syria

Admin.WagnerD21 Agosti 2013

Majeshi ya Syria leo hii yameshambulia vikali kwa kutumia mizinga na maroketi katika baadhi ya viunga vya jiji la Damascus, shambulio ambalo makundi mawili ya upinzani yanadai imetumika hewa ya sumu na kusababisha vifo.

https://p.dw.com/p/19Txt
People, affected by what activists say is nerve gas, are treated at a hospital in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists accused President Bashar al-Assad's forces of launching a nerve gas attack on rebel-held districts near Damascus on Wednesday that they said killed more than 200 people. There was no immediate comment from Syrian authorities, who have denied using chemical weapons during the country's two-year conflict, and have accused rebels of using them, which the rebels deny. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CONFLICT)
waathirika wa kinachodaiwa kuwa sumuPicha: Reuters

Madai hayo yanatolewa wakati timu ya watu 20 ya Umoja wa Mataifa ikiwa nchini Syria kwa ajali ya kuchunguza madai ya kutumiwa silaha za kemikali katika miji mitatu tofauti nchini humo ambayo inadaiwa kutumika silaha hizo za maangamizi.

Hata hivyo serikali ya Syria imeibuka na kukanisha vikali madai hayo ya kutumia silaha za kemikali katika shambulizi hili la sasa. Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa hilo SANA, likinukuu chanzo ambacho hakukutaka kutaja jina lake kikisema "Taarifa hiyo ni jaribio la kupoteza malengo ya timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kutekeleza vyema wajibu wake".

Uzito wa mashambulizi

Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu la Syria lenye makao yake mjini London, limesema mashambulizi yalikuwa makali sana na yalilenga viunga vya Damascus kwa upande wa mashariki, maeneo ya Zamalika, Arebeen na Ein Tarma.

Free Syrian Army fighters walk past damaged buildings and debris in Deir al-Zor August 20, 2013. Picture taken August 20, 2013. REUTERS/Khalil Ashawi (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS CIVIL UNREST)
Waasi wa Syria wakitembea katika eneo lililovurugwaPicha: Reuters

Katika taarifa yake shirika hilo limemnukuu, mwanaharakati akisema majeshi ya serikali yamefyatua mareketi yenye hewa ya sumu, na kuuwa watu kumi. Rami Abdul-Rahman, mkuu wa shirika hilo alitilia mkazo kauli hiyo kwa kusema wamepata taarifa za kufyatuliwa hewa ya yenye sumu kwa kumia maroketi sambamba na maeneo mengine ya angani.

Kundi lingine la wanaharakati limesema mamia ya watu wameuwawa au kujeruhiwa kufatia kutokana na mashambulizi hayo. Kuwepo kwa takwimu tofauti za vifo au majeruhi kutoka nchini Syria imekuwa kawaida unapotokea mkasa kama huo kwa kuwa kuzuia waandisha wa nje wa ndani kuripoti kuhusu mambo yanayojitokeza.

Zaidi ya watu 40 wameuwawa

Abdul-Rahman amesema zaidi ya watu 40 wamethibitishwa kuuwawa na kwamba vifo hivyo vitegemewe kuongeza mpaka kufikia watu 200 katika vitongoji vya jiji la Damascus.

*** Bitte Richtlinien im DW-Journalistenhandbuch konsultieren **** ATTENTION EDITORS - VISUALS COVERAGE OF SCENES OF DEATH AND INJURY Syrian activists inspect the bodies of people they say were killed by nerve gas in the Ghouta region, in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists said at least 213 people, including women and children, were killed on Wednesday in a nerve gas attack by President Bashar al-Assad's forces on rebel-held districts of the Ghouta region east of Damascus. REUTERS/Bassam Khabieh (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS CIVIL UNREST) TEMPLATE OUT
Baadhi ya watu waliuwawa katika eneo la GhoutaPicha: Reuters

Serikali imekanusha madai ya upande wa upinzani kwamba inatumia silaha za kemikali, kwa kusema waasi wanaopigana kumuondoa Bashar al Assad wamewahi kutumia silaha hizo.

Kufuatia repoti za leo hii, wanaharakati wametoa wito kwa timu ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Syria kwa sasa na asasi nyingine za kimataifa kufika katika maeneo yalikufanyika mashambulizi kwa lengo la kufanikisha haraka upatikanaji wa matibabu na misaada mingine ya kiutu pamoja na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi hilo.

Mwanaharakati mwingine katika eneo hilo Mohammed Said amesema idadi kubwa watu walikufa na majeruhi imewahishwa katika hospitali moja iliyopo mashariki mwa viunga vya Damascus.

Madai haya ya leo ya kutimika kwa silaha za kemikali kama yatathibitishwa litakuwa tukio kubwa zaidi kufanyika zaidi ya lile la Machi 19 katika eneo la Khan al-Assal ambalo zaidi ya watu 30 walipoteza maisha na upande wa Assad na waasi wanalaumiana kufuatia shambulio hilo.

Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhriri:Yusuf Saumu