Sudan yafungua tena anga lake
15 Januari 2020Ghasia hizo zilikuwa makabiliano makubwa kuwahi kufanyika kati ya maafisa hao wa zamani wa usalama na waungaji mkono wa utawala mpya, ambao ulisaidia kumuangusha kutoka madarakani Bashir mwezi Aprili baada ya miaka 30 akiwa madarakani. Kiongozi wa baraza la mpito Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema jeshi la nchi hiyo linaudhibiti wa majengo yote ya idara ya usalama wa taifa.
Katika hotuba mapema leo, kiongozi wa baraza linaloongoza nchi hiyo, luteni jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliapa kutoruhusu mapinduzi yoyote kutokea nchini humo. Maafisa wa zamani wa usalama wa taifa walipambana katika mji mkuu Khartoum, kwa masaa kadhaa hadi pale majeshi ya serikali yalipozima uasi huo jioni ya jana, kulingana na wakaazi na duru za kijeshi.