1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan iko njia panda kukijumuisha kikosi cha mgambo jeshini

Saumu Mwasimba
28 Juni 2021

Serikali ya mpito ya Sudan inakabiliwa na kizingiti katika hatua ya kukijumuisha jeshini kikosi maalum cha mgambo chenye nguvu nchini humo.

https://p.dw.com/p/3vhEt
Äthiopien I  Sudan I Konflik
Picha: Mahmoud Hjaj/Anadolu Agency/picture-alliance

Serikali hiyo ya kijeshi na kiraia iko madarakani tangu mwaka 2019 chini ya mpango wa makubaliano ya kugawana madaraka.

Awali serikali hiyo ilitarajiwa kumaliza  muda wake mwaka ujao lakini iliongezewa muda baada ya kufikiwa makubaliano ya amani mwezi Oktoba na makundi ya waasi.

Makubaliano hayo yaliweka wazi haja ya kufanyika mageuzi katika jeshi ikiwemo hatua ya kukijumuisha kikosi maalum cha jeshi la mgambo kilichoundwa mnamo mwaka 2013 kwa ajili ya kukabiliana na waasi waliokuwa wakipambana na serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Omar al Bashir, nchi nzima.

Katika kipindi cha wiki kadhaa kumeripotiwa kuwepo mvutano mkubwa kati ya kikosi hicho cha mgambo na jeshi la taifa, lakini wasiwasi umeongezeka zaidi baada ya kamanda wa kikosi hicho cha mgambo, Mohammed Hamdan Daglo, kukataa hadharani kujumuishwa kwa kikosi chake jeshini.