1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Streich amwaga wino Freiburg

Josephat Charo
9 Machi 2022

Christian Streich ndiye kocha aliyefanya kazi kwa muda mrefu kabisa katika ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga.

https://p.dw.com/p/48BMP
Fußball Bundesliga FC Bayern München - SC Freiburg
Picha: Sascha Walther/Eibner/imago images

Kocha wa klabu ya Freiburg, Christian Streich, ambaye ndiye kocha aliyehudumu kwa muda mrefu katika ligi ya soka ya Ujerumani, Bundesliga, amerefusha mkataba wake kwa mara nyingine. Freiburg haikutoa maelezo yoyote lakini imesema Jumanne kuwa Streich, mwenye umri wa miaka 56, ataisimamia timu hiyo msimu ujao.

Streich, ambaye aliwahi kurefusha mkataba kwa mwaka mmoja, amekuwa akiikufunzi Freiburg tangu Desemba 2011 na amesimamia mechi 383 katika mashindano yote. Alijiunga na klabu hiyo mnamo 1995 kama kocha wa timu ya vijana.

Freiburg wanafurahia msimu wakiwa imara, wakiwa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na katika eneo la kuwania nafasi ya kufuzu moja kwa moja kwa michuano ya kombe la mabingwa Ulaya, Champions. Freiburg pia imetinga nusu fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani ambapo itakwaana na HSV Hamburg mwezi Aprili.

"Tumejenga msingi imara katika miaka ya nyuma uliojikita katika uaminifu na kazi kwa bidii," alisema mkurugenzi wa michezo, Jochen Saier.

"Tumeshawishika kwamba tunaweza kuendelea kufanya kazi kwa mafanikio katika maendeleo ya timu yetu katika msingi huu," aliongeza Saier, wakati Freiburg iliporefusha pia mikataba ya makocha watatu wasaidizi.

(dpa)