Strauss-Kahn aachiwa kwa dhamana | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Strauss-Kahn aachiwa kwa dhamana

Aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Fedha Dunia -IMF- ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya ubakaji Dominique Strauss-Kahn, ameachiliwa kwa dhamana na Jaji wa mahakama ya mjini New York Marekani.

default

Dominique Strauss Kahn

Dominique Strauss-Kahn, ameachiliwa kwa dhamana baada ya kusota rumande kwa siku tano.

Hata hivyo ametakiwa kubakia mjini New York, baada ya kutoa fedha taslim, dola milioni moja na kuwekewa bima ya dhamana ya dola milioni tano.

Dominique Strauss-Kahn Gericht IWF 19.05.

Dominique Strauss-Kahn akiwa mahakamani

Dhamana hiyo imekuja baada ya  jopo la majaji kumfungulia mashtaka saba dhidi yake juu ya tuhuma za jaribio la kumnyanyasa kimapenzi na kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli ya Manhattan jumamosi iliyopita.

Tuhuma ambazo Strauss-Kahn mwenyewe amesema atapambana nazo.

Wakati huohuo, uamuzi wa kujiuzulu kwa Mkurugenzi huyo mtendaji wa -IMF- umeibua mjadala kuhusu ni nani anayeweza kumrithi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anataka tena mtu kutoka

barani Ulaya kuongoza chombo hicho, wakati China, ikiunga mkono miito ya mataifa ya bara la Asia ya kumchagua kiongozi mpya kutoka taifa linaloinukia kiuchumi.

DW inapendekeza

 • Tarehe 20.05.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza (ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11K6u
 • Tarehe 20.05.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza (ZPR)
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11K6u

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com