1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stockholm. Upepo mkali waikumba Sweden.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaH

Upepo mkali umeshambulia na kuharibu sehemu kadha kusini mwa Sweden, na kuuwa kiasi watu watatu, na kuharibu utaratibu wa usafiri na kuwaacha kiasi watu 270,000 wakiwa hawana umeme.

Wahanga hao wote walifikwa na umauti baada ya kuangukiwa na miti. Huduma za reli zimesimamishwa kwasababu miti imeangukia katika njia za reli. Barabara na usafiri wa anga pia nao umeathirika sana.

Magari yamepigwa marufuku kupita katika daraja linalounganisha Sweden na Denmark. Huduma za feri kutoka Sweden bara pia zimefutwa.